![]() |
Mwanamuziki na Mtayarishaji Midundo,Man Walter{Shati jeupe} akiwa na Msanii 20%. |
Mtayarishaji wa muziki kutoka Studio za Combination Sound, Man Walter aliwahi kutangaza kumaliza tofauti kati yake na msanii 20 Percent aliyewahi kufanya vizuri kupitia mikono yake na kwa pamoja wakaeleza mpango wa kufanya mradi mpya. Man Water ameongea na kueleza walipofikia baada ya ukimya wa muda mrefu tangu walipotangaza hatua hiyo. “Off Course kwa sasa siwezi kuongelea sana kwa sababu wazo lilienda vizuri lakini nadhani kuna vitu viwili vitatu vilikwama, sijapata tena mawasiliano mazuri na 20. Labda tuvute subira tu, kwa sababu kama watu wana lengo la kufanya jema litakuwa tu…nadhani tuvute subira kwake. Amefafanua kuwa milango iko wazi kwa 20 Percent kufanya kazi kwake kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara lakini pia anasubiri sana kufanya kazi na msanii huyo ili kuwahakikishia watu kuwa hakuna tatizo lolote kati yao. 20 Percent aliwahi kuchukua tuzo 5 katika kinyang’anyiro cha KTMA kwa kazi alizofanya na Man Walter. Man Walter ameachia wimbo mpya hivi karibuni aliofanya mwenyewe kwa kushirikiana na msanii anayejulikana kwa jina la Mbatizaji. wimbo Unaitwa ‘Wife Material’.
No comments:
Post a Comment