Wednesday, 10 September 2014

MAUZAUZA YAANZA BAADA YA AJALI YA MARA.


Kaburi la mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi ya Mwanza Coach na J4 katika eneo la Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana leo asubuhi. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya Musoma , ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanye mazishi, ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika kuhifadhi mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni.
Mwili wa marehemu bado uko ndani,Huku watu wengi wako hapa na polisi wameimarisha hali ya usalama. Madaktari wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu. Inasikitisha sana. Kimeeleza chanzo chetu cha kuaminika. Ijumaa iliyopita, kulitokea ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, mabasi ya kampuni ya Mwanza Coach na J4 pamoja na gari dogo aina ya Toyota-Landcruiser. Ambapo Watu zaidi ya 40 walifariki dunia na wengine 79 kujeruhiwa.

No comments: