Tuesday, 9 September 2014

PICHA-Mwigizaji mkongwe nchini Lucy Komba afunga ndoa rasmi.


Atimaye yule muigizaji mkongwe nchini Lucy komba amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi aishie nchini Denmark anayefahamika kwa jina la Stanley,. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii nchini lucy ameandika maneno haya kuashiria tukio hilo "..Asante Mungu kwa siku hii nzuri na muhimu sana katika maisha yangu, wengi hawakutaka nifikie siku hii, kuna wengine walinuna, kuna wengine waliniombea mabaya, kuna wengine walichukia na wengine waliambiana wanichunie walifikiri bila wao Mungu hawezi kuifanikisha siku hii, nasema asante Mungu kwa sababu uliifanikisha siku hii kwa nguvu zako watu wanaonipenda walisheherekea siku hii vizuri walikunywa na kula na kusaza watu zaidi ya mia sita walikuwa ukumbini wakishangilia pamoja nami haleluyaaaaaaaaaaaaaaa anachokiunganisha Mungu binadamu hawezi kukitenganisha hata iweje.."anamalizia Lucy...
Hizi hapa chini ni baadhi ya picha za kumbukumbu ya Ndoa yake,



SISI KAMA..https://www.ngessa blogspot.com TUNAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA UNGANIKO LAO LA MAISHA,NA BARAKA ZA MUNGU ZIWANYESHEE KAMA MVUA.

No comments: