Friday, 10 October 2014

Jambazi sugu lenye kuwaibia na kuwaua wanawake Arusha lauawa!


Wadau habari zilizovuma siku chache jijini Arusha ni matukio yenye kufanana ya kuporwa,kujeruhiwa na hata kuuawa kwa wanawake mkoani Arusha. Matukio haya yaliwastua wengi sana kwani haikujulikana wazi kuwa ni ujambazi,visasi ama mauaji ya kupanga lakini habari za hivi punde ni kwamba mpanga matukio hayo yote Bw,Ramadhan Abdallah a.k.a Ramadhan Ndonga(master mind) ameuawa na jeshi la polisi eneo la Moivo Sanawari ya juu na hivi sasa wananchi wamejazana kituo kikuu cha polisi Arusha wakiutizama mwili wa muuaji huyo aliyeikosesha Arusha raha kwa muda sasa.
Mwili wa marehemu Ramadhan Abdallah"Ndonga"

HOFU iliyokuwa imetanda katika mkoa wa Arusha na viunga vyake kwa hivi sasa inaelezwa kuwa huenda ikawa shwari baada ya mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la, Ramadhan Abdallah Jumanne, ambaye amekuwa akiwaua kwa kuwapiga risasi wanawake mbalimbali jijini Arusha,
Wananchi wakiwa wamekusanyika Polisi-Kituo cha Kati Arusha kushuhudia mwili wa jambazi hilo.

kuuwawa katika mapambano ya kurushiana risasi na Polisi. Polisi wamekuwa wakimtafuta mtu huyo kwa muda mrefu kwa tuhuma za mauaji wanawake pamoja na watu mbalimbali ambapo usiku wa kuamkia leo Octoba 10, 2014 ameuwawa katika majibizano hayo. Polisi mkoani humo wamekaririwa na wakisema, mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa Moivo jijini humo alifanya uhalifu jana Octoba 9, 2014 mchana na kuanza kumfuatilia na kugundua anapoishi.
Kamanda wa Polisi-Arusha Liberatus Sabas akitoa ufafanuzi juu ya tukio hilo,ikiwemo kuzionyesha silaha kali alizokamatwa nazo jambazi huyo.

Wamesema baadae walikwenda nyumbani kwake majira ya saa nane usiku kwa lengo la kumkamata lakini alianza kurusha risasi na kutoka nje ndipo Polisi walipojibu mapigo na kumjeruhi na alikufa akiwa njiani kupelekwa hospitali ya mkoa huo Mount Meru kwa matibabu. Attachment 192076 Watu wengi hususani wanawake walifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha kumtambua mtu huyo, na wengi wao walimtambua kwamba aliwafanyia vitendo vya uhalifu.
 Aidha, taarifa zinasema vitu alivyokutwa navyo baada ya kufanyika kwa upekuzi nyumbani kwake ni pamoja na bastola na magazini nne zenye uwezo wa kubeba risasi kwa viwango tofauti ikiwemo yenye kubeba risasi 30, Radio ya upepo ya Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya Rwanda, pikipiki mbili zenye namba tofauti na Polisi inamtafuta mwendesha pikipiki huyo kwa kuhusika na uhalifu.
Silaha zilizokamatwa Nyumbani kwa Jambazi hilo.
Kumbukumbu zinaonyesha kwamba sakata la aina mpya ya mauaji yaliyoibuka hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo miji mikuu, yalichukua maisha ya watu wasio na hatia na wengine kupata ulemavu wa kudumu pasipo msako wa kuwatafuta wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria. Attachment 192077 Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha Agosti 7, 2014 ilisema kumekuwepo na matukio mawili ya kuvamiwa kwa wanawake na kujeruhiwa kwa risasi na mara baada tu ya kufanyika kwa mauaji hayo wahusika wanatokomea kusikojulikana bila kubeba kitu chochote. Tukio la kwanza lilitokea eneo la Sakina kwa Iddi ambapo Flora Porokwa (37) ambaye ni mke wa Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wafugaji la Pingos Forum, Edward Porokwa, mkazi wa eneo hilo alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wakitumia usafiri wa pikipiki na kumfyatulia risasi na kumjeruhi akiwa ndani ya gari yake kisha kutokomea kusikojulikana. Attachment 192078 Hata hivyo, katika tukio la pili mwanamke mwingine, Samimu Rashidi (30), alivamiwa Agosti 6 mwaka huu, usiku saa 3 na kupigwa risasi ya shingoni na kufa akiwa ndani ya gari lenye namba T.569 BAY aina ya Toyota katika eneo la makao mapya jijini humo.

No comments: