Friday, 31 October 2014

SHYROSE BANJI NA "MSALA" MWINGINE BUNGENI

Mh,Shyrose Banji{Mb}

MVUTANO mkubwa unaoendelea ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) umekwamisha shughuli za Bunge hilo kutokana na baadhi ya wabunge kugomea, wakitaka kwanza Mbunge kutoka Tanzania, Shyrose Bhanji achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kile wanachodai kuwa ni utovu wa nidhamu.
 Shyrose, anatuhumiwa kutoa lugha chafu kwa baadhi ya wabunge wenzake na viongozi wakuu wa nchi za Rwanda, Uganda na Kenya, wakati wa ziara ya viongozi wa EALA iliyofanyika Brussels, Ubelgiji wiki mbili zilizopita. Kutokana na tuhuma hizo, wabunge wenzake wanamshinikiza Spika wa EALA, Margaret Zziwa aruhusu mjadala kuhusu Shyrose, lakini kiongozi huyo hakuwa amekubaliana na suala hilo, hivyo kusababisha miswada ya sheria na taarifa za kamati ambazo zilipangwa kujadiliwa na vikao vya Bunge hilo kuwekwa kando.

No comments: