Wednesday, 1 October 2014

WEMA SEPETU AZAWADIWA GARI MBILI KWENYE BIRTHDAY PARTY YAKE.

Wema Abraham Sepetu katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Miss Tanzania 2006 ambaye bado analinda jina lake lisipotee midomoni mwa watu Wema Abraham Sepetu, ameshangazwa na watu wake wa karibu kwa zawadi alizopokea katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake. Wema alipokea gari mbili ambapo moja alipewa na Mpenzi wake Chibu Dangote "Diamond Platnumz" aina ya Nissan Murano ipo hapo chini pamoja na BMW ambayo hii wengi hawakujua imetoka kwa nani lakini baadae ukweli ulitambulika kuwa imetoka kwa Manager wake mbunifu wa mitindo nchini Martin Kadinda. Martin amemkabidhi Wema gari hilo pamoja na kadi ya Gari ikiwa imeandikwa jina lake.
Gari aina ya NISSAN{MURANO}ambayo Wema amezawadiwa na mpenziwe Diamond Platnumz kama zawadi ya Birthday.
Meneja wa Wema Abraham Sepetu,Martin Kadinda akimkabidhi Wema Sepetu kadi ya gari aina ya BMW kama zawadi ya Birthday.
Wema akishangaa zawadi ya gari aina ya BMW aliyozawadiwa na Meneja wake Martin Kadinda.

No comments: