Breaking News: Msanii maarufu wa Hip Hop nchini Geez Mabovu afariki dunia
 |
Geez Mabovu |
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Iringa, Geez amefariki jioni ya siku ya jana.Taarifa zinadai kuwa Geez Alienda kwao
wiki moja na nusu iliyopita ambako alianza kuugua mfululizo mpaka mauti
yalipomkuta.
Geez atazikwa (Leo) jioni November 13 2014.
No comments:
Post a Comment