![]() |
Marehemu Geez Mabovu |
Geez Mabovu hatunae Tena.Geez Alifariki juzi Majira ya Saa moja usiku huko mkoani Iringa ambapo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya Figo.
Moja kati ya Marafiki wa Karibu wa Geez Mabovu ambaye pia ni mwanamuziki wa siku nyingi Dark Master Kutoka Kundi la "Chamber Squad" ameonyesha kuguswa mno na kifo cha rafiki yake huyo ambapo hapo kabla aliwasili mapema mkoani Iringa ili kujua maendeleo ya afya yake.
Dark master alikuwepo mkoani Iringa Tangu Siku ya Jumamosi na alifanikiwa kumjua hali mara kadhaa kabla ya hali yake kubadilika na kuacha wanafamilia wakishughulikia matatizo yake kifamilia.
Dark Master alisema kuwa baada ya hali ya Geez kubadilika siku chache zilizopita Mzee wa Geez aliwaita ndugu wa karibu na marafiki wake wa karibu sana waje kumuona kwa mara ya mwisho ingawa walihisi ni wasiwasi tu wa mzee huyo
"Mzee alitupigia simu tuje kumuona kwa kua alihisi hali yake ni mbaya na hatopona ingawa sisi hatukuamini nikawahi kwenda kumuona tangu jumamosi niko Iringa kumuona mshikaji wangu lakini sasa najiandaa kumzika kikubwa tumuombee tu kwa Mungu sababu hakuna anayejijua atakufaje "alisema Dark Master
Dark Master ni Rafiki mkubwa wa Marehemu Geez Mabovu ambaye jina lake halisi ni Ahmed Upete na alifanikiwa kufanya naye wimbo ulioitwa Dakika Sifuri ambao pia walishirikana na Hayati Albert Mangwea.
Geez Mabovu amezikwa jana majira ya saa kumi jioni mkoani Iringa

No comments:
Post a Comment