![]() |
Mh,JANUARY MAKAMBA. |
SIKU moja kupita baada ya Ripoti ya utafiti uliondaliwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya TWAWEZA kumpa nafasi kubwa Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond,
Edward Lowassa kwamba ndio anayefaa kumrithi Rais anayemaliza mda wake
Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2015 na kuwapiku wanasiasa
wengine ikiwemo Waziri mkuu Mizengo Pinda na wengine ndani ya chama cha Mapinduzi CCM ,
Sasa Ripoti hiyo imeanza kupingwa na wadau mbalimbali ikwemo wasaka
urais ndani ya chama cha mapinduzi CCM,na kusema ripoti hiyo imejaa
ubabaishaji mtupu wenye lengo wakuwadanganya watanzania kuwaamini kwamba
viongozi hao ndio wanafaa kumbe sio kweli.
Akipinga Ripoti hiyo ya TWAWEZA waziwazi, ni Naibu Waziri wa
Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Jannuary Makamba ambaye amesema hata
utafiti wenyewe umejikita sehemu moja tu tena mjini na haujafika hata
katika visiwa vya unguja na pemba na misingi hiyo inazidi kuushusha
hazi utafiti wenyewe.
Makamba
ambaye ni Miongoni mwa wasaka urais kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi
ambaye amejiapiza kufa na kupona kushika nafasi ya kumrithi Rais
anayemaliza mda wake Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumza na Redio ya Magic Fm katika kipindi cha Morning Magic,
Ambapo alizidi kwenda mbali zaidi huku akionekana akimbeza Msaka Urais
Mwenzake kutoka chama cha Mapinduzi CCM na mbunge wa monduli Edward
Lowassa,na kusema inasikitisha kuona kuwa mtu zaidi ya miaka kumi akiusaka
urais na watanzania wanamjua leo nafasi yake imeshuka sana kupitia
utafiti huo,
Makamba ambaye Vilevile ni kiongozi kijana kutoka ccm,aliendelea kusema Chama cha Mapinduzi
{CCM} kinasifa 13 wakati wa kumteua mgombea wa urais ambazo ziliwekwa
tangu mwaka 1985 ambapo sifa hizo zipo wazi ikiwemo sifa za uadilifu,
Vilevile Makamba akatolea mfano 1995 ambapo wakati wa wakumtafuta
mgombea kupitia CCM, walitumia sifa hizo na wakati huo walikuwepo
wanasiasa maarufu,ila wakati wa kwenda Mkoani Dodoma na Wagombe hao
maarufu wakakataliwa na CCM na akachaguliwa mgombea ambaye ni ajulikani
kabisa na akasema kuwa CCM haichagui kiongozi kutokana na Umaharufu kama
aliyokuwa nao Lowassa.
Kwa upande wake mwandishi wa Habari kutoka Redio Maria Joseph
mwalukusa alisema ripoti hiyo inamakosa mengi kwani imewaaangalia watu
wa mijini tu na kuwaacha watu wavijijini na akaongeza kuwa ni wazi
kutakuwa na njama zinafanywa ili kumbeba mtu ambaye anarekodi za uchafu
ili achaguliwe na watanzania
No comments:
Post a Comment