Mwanamuziki
wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro
Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au
kulipa faini ya shingili laki tisa baada ya kupatikana na hatia ya
makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye
thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo
kijiko na kigae.
Taarifa
zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa nguli huyo wa muziki wa Hiphop
amefanikiwa kulipa faini hiyo na sasa yuko huru kuendelea na mambo
mengine ya kulijenga taifa ikiwemo shughuli zake za kimuziki.

No comments:
Post a Comment