![]() |
| Mh,Temba. |
Msanii
kutoka TMK Wanaume Family, Amani James aka Mh Temba jana amefikishwa
katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es salaam akikabiliwa na
mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi.
Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake mbele ya hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo.
Mheshimiwa
Temba alifikishwa mahakani hapo mapema saa 3:00 asubuhi huku akiwa
amefungwa pingu chini ya ulinzi wa askari kanzu wa kituo cha Mkoa wa
Kipolisi Chang’ombe.
Aliwekwa
chini ya ulinzi katika kituo cha mahabusu ya mahakama hiyo kabla ya
kusomewa mashitaka yake. Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba
371 chini ya kifungu cha 89 kidogo cha (2) (a) sura ya 16 ya mwenendo
wa sheria ya Makosa ya Jinai.
Akisomewa
mashitaka na karani wa mahakama hiyo, Joyce Ngamesha, alidaiwa kuwa
Januari 28, mwaka huu, saa 1:00 jioni katika baa ya Scorpion Iiliyopo
Temeke jijini Dae es salaam, mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu Godfrey
Deogratius ama Sulla.
Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yupo nje kwa dhamana.
Hakimu
Frank alisema kesi hiyo itasikiliza ushahidi March 11, mwaka huu,.
Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mshitakiwa alifikishwa katika kituo
cha polisi cha Chang’ombe akituhumiwa kutishia kumchoma kisu
mlalamikaji kwa madai ya kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mke wa msanii
huyo.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu mlalamikaji huku akijua ni kinyume na sheria.
Source-NIPASHE.

No comments:
Post a Comment