Wakati mwanamziki wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz akiendelea kupepesa
macho na kutikisa masikio kukanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na
mwingizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ukaribu wao bado unatia mashaka
na kuendeleza sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wapambe wao.
Japo kuwa Ommy alieleza kuwa yeye na Wema ni marafiki toka kitambo kabla hata ya wema kuwa na mahusiano na mwanamziki Diamond, lakini hii sasa imezidiii.
Mbali na kuonekana pamoja sehemu mbalimbali za starehe toka Ommy atoke Marekani, hili la kupikiwa na kupakuliwa nyumbani kwa Wema tena mida ya usiku ndio limezidi kuchochea hisia kuwa wawili hao wanamahusiano zaidi ya USHIKAJI.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwanadada Wema ambaye ana followers zaidi ya laki nne , alibandika picha hiyo hapo juu akionekana kumpakulia chakula ambacho alijisifia ni kizuri na amekipika mwenyewe na kumtania Ommy kuwa alikuwa analeta pozi kwenye kula.
“Dat moment anapokuja home and umepika chakula alafu analeta pozi at first then unashangaa anaenda sahani mbili.... Talk About Good Food Made Real Good”- Wema aliandika mara baada ya kutupia picha hiyo.
Japo kuwa hadi sasa mwanadada Wema Sepetu ajajitokeza kukataa au kukubali juu ya yeye kuwa na mahusiano na Ommy lakini idadi kubwa ya wapambe wake mitandaoni wametokea kuifagilia sana hii “Couple”.
Tuvute subraaa.
Mzee wa Ubuyu

No comments:
Post a Comment