Monday, 16 February 2015

Msanii Judith Wambura 'Lady Jaydee' aeleza juu ya umiliki wa EFM Radio 93.7

Maswali yamekuwa mengi kwa mwimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchin Judith Wambura 'Lady Jaydee' juu ya maisha yake ambapo aliulizwa juu ya kuachana na mumewake lakini pia kuhusiana na kufungua kituo cha matangazo kwa njia ya sauti (Radio) na au umiliki wa EFM Radio inayo patikana kwenye masafa ya 93.7 Fm jijini Dar es Salaam.

Haya ndiyo aliyo sema kupitia account yake ya Instagram.
Ulituahidi utafungua Radio mbona kimya mpaka leo?
JIBU : "Niliandika hiyo kitu siku ya wajinga duniani, April 1, sikuwahi kuahidi. 
Lakini matamanio yangu ni siku moja kumiliki kituo cha radio na ikibidi hata television. 
Hakuna linalo shindikana, palipo na nia. ������������������������ EFM radio ni yako? 
JIBU : Hapana sio yangu 
Nafikiri inadhaniwa hivyo kutokana na kila mtu ku tamani, mimi niwe na radio. 
Je!mtaniruhusu na mimi niwaulize swali? ???������������
Kwanini mnatamani sana niwe na radio? ?
Mungu akijaalia ntakuwa nayo ���������������� ☝☝☝☝☝☝" Ameandika Lady JayDee.

 

No comments: