Wednesday, 25 February 2015

TASWIRA ZA MAZISHI YA MAREHEMU MEZ B { DODOMA}

Marehemu msanii Mez B enzi za uhai wake.
Msanii Mez B aka Moses aliyekuwa Mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kurudishwa nyumbani na mama yake mzazi amefariki Dunia siku ya juzi mkoani humo. Mez B alikuwa akiuguliwa na homa ya mapafu [TB] na alikuwa kwenye dozi huku siku aliyoaga dunia ilikuwa siku ya tatu toka anatumia dawa hizo.
siku aliyofariki Mez B aliamka na kunywa dawa na chakula ila hali yake haikuwa sawa na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa simu na kuamuru awekewe drip ila hali yake haikutengamaa, wakati wanampeleka hospitalini alifia  mapokezi.
Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen.
NB-Na Hizi ni PICHA zikionyesha taswira halisi ya Mazishi ya msanii Mez B mkoani Dodoma,
Mama mzazi wa Mez B, Marry Mkandawile (katikati) akiwa ameshikiliwa na ndugu baada ya kuingia viwanja vya Mashujaa ili kutoa heshima za mwisho.

Wananchi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Marehemu Mez B baada ya kuagwa na mashabiki wa mziki pamoja na ndugu jamaa na marafiki mwili wake ulielekea kupumzishwa katika makaburi ya Wahanga Maili mbili


Baadhi ya wasanii waliohudhuria msiba wa Mez B wakiwa kwenye majonzi mazito

Mtangazi wa Citizen TV anayejulikana kwa jina la Mzazi Willy Tuva akifanya mahojiano na msanii wa Bongo Fleva Dogo Janja"Janjaro".

 

No comments: