Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha
kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp
Kardinali Pengo.
Akiongea kabla ya kuhojiwa na polisi Mchungaji Gwajima amejitetea kuwa alichofanya ni kutumia fursa ya kumuonya kiongozi mwenzake wa kiroho kutokana na kuwageuka wenzake katika makubaliano waliofikia katika tamko la kuipigia kura ya hapana Katiba inayopendekezwa.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kumkadhifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo. Inadaiwa matusi hayo yameonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya WhatsApp na mingineyo, ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.

No comments:
Post a Comment