Monday, 13 July 2015

MAJAMBAZI WAVAMIA KITUO CHA POLISI STAKI SHARI NA KUUA SABA WAKIWEMO ASKARI POLISI.

Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi Sitakishari. Ukonga. Dar tukio lililotokea saa 5 usiku wa kuamkia leo, jumla ya waliokufa ni 7. Wakiwemo Askari polisi wanne, mgambo 1, na raia 2.
Kati ya raia, mmoja ni mtuhumiwa mwanamke aliyepelekwa na mgambo ambaye naye ameuawa na mwingine kujeruiwa.
Majambazi hao wamefanikiwa kupora Bunduki aina SMG 15 na Radio call 1

Mbona imekuwa kama ni kawaida kwa majambazi kuvamia vituo vya polisi na kuua ikiwemo kupora silaha zilizopo kwenye vituo vya Polisi?baada ya kuziiba hizo silaha wanazipeleka wapi?
kazi kwenu.‪#‎jeshi‬ la polisi#wizara ya mambo ya ndani#usalama wa taifa.ili ni tatizo linaloelekea kuwa sugu,na ukweli ni kwamba sisi raia tulio huku uswahilini tunaishi kwa hofu kubwa.....

 

No comments: