Bondia Mohamed Matumla amefanikiwa kutoka kimasomaso baada
ya kumchapa kwa points bondia mwenzake kutoka nchini China Wang Xin
Hua katika mpambano wa raundi 10 uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee jana usiku.
Mpambano huo ulikuwa ni wakuwania nafasi ya kucheza katika
pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na
wapenzi wengi wa masumbwi duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr.
na Manny Pacquiao unakaochezwa mapema Mei 2, mwaka huu, huko Las Vegas,
Marekani.
No comments:
Post a Comment