Wednesday, 4 March 2015

PICHA:-MAZISHI YA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA-LITUHI-NYASA{RUVUMA}

Marehemu Kapteni John Komba amezikwa jana March 03 kwenye makaburi ya Mission yaliyopo Kijijini kwao Lituhi ambapo mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyoanza saa 5 asubuhi na mazishi yalikamilika saa 10 jioni,




Ibada ya sala iliongozwa na Askofu wa Jimbo kuu la Mbinga Askofu John Ndimbo na kuhudhiriwa na Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete,Spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda,wabunge mbalimbali,pamoja na viongozi wa dini pamoja na wananchi.

Spika wa Bunge la Tanzania Bi. Anna Makinda

Kutoka kambi pinzani,Mbunge wa Lindi Salum Baruani.

Katibu wa CCM Abdulrahman Kinana




Mh,Rais J.M.Kikwete akiongea jambo muda mfupi baada ya Maziko kijijini Lituhi-Nyasa{Ruvuma}


Mama Salma Kikwete akiwa amekaa karibu na mke wa Marehemu Komba,Bi Salome Komba.


Aliyekua Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapten John Komba jana alipumzishwa kwenye makazi yake ya milele ambapo Mazishi yake yalihudhuriwa na idadi kubwa ya Watanzania  kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania ambao walikusanyika kwa ajili ya kumsindikiza kwenye safari yake hiyo ya mwisho.



Mke wa Marehemu Bi,Salome Komba.


Makamu wa Kwanza wa Rais Dr Ghalib Bilal akiweka Shada la Maua.

No comments: