Thursday, 12 March 2015

PICHA:-Sabby, Cyrill Kimalovee Zaidi.

Mrembo na staa wa Bongo Movie, Sabrina Omary ‘Sabby’  na Mkali katika muziki wa Bongo Fleva, Cyrill Kamikaze hivi karibuni walinaswa katika ufukwe wa Hoteli ya Golden Tulip, Masaki jijini Dar wakiwa kimahaba na hivyo kuzidisha tetesi kuwa wanatoka kimapenzi.
Chanzo makini toka GPL kilisema wawili hao walionekana hotelini hapo wakiwa eneo la kuogelea na walipomaliza walihamia katika viti ambako sasa walikumbatiana kimahaba kana kwamba hakuna mtu anayewaona.
Kwa nyakati tofauti walipoulizwa kuhusu tetesi za kuwa wapenzi na ushahidi wa picha, kila mmoja alikana, wakidai zitakuwa ni picha za kutengenezwa kwa sababu mchezo huo umekuwa maarufu siku hizi huku Sabby akisisitiza kuwa angefika ofisi za GPL ili kujiridhisha na picha hizo ndipo aweze kuzungumza, kitu ambacho hakukifanya
Source-GPL

No comments: