Mwanamuziki
wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepondwa vibaya katika
msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba,
baada ya kuvaa kigauni kilichombana na kumuonyesha maungo yake ya mwili
mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
![]() |
| Mwanamuziki wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba pamoja na wasanii wenzake kwenye msiba wa Komba. |
Baadhi
ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta jijini
Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo kujitokeza mbele
na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni alichovaa
bi’dada huyo.
“
Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo tofauti na wenzake
ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri maumbo yao, kwa nini
yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye alikuwemo kwenye maombolezo.
Mwandishi
wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza kuhusiana na hilo alisema hakuvaa
vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na umbo la mwili wake.


No comments:
Post a Comment