Wednesday, 25 March 2015

USHAHIDI-MAREHEMU KANUMBA & RAY NDIO WAANZILISHI WA KUCOPY NA KUPASTE MOVIE[BONGO MOVIE]

Mcheza filamu za kibongo ambaye pia ni muigiazaji wa michezo ya kuigiza kupitia kituo cha televisheni cha Chanel Ten, Rachel Silvestar  amesma anashangazwa na baadhi ya watu kumchukulia vibaya muigizaji mkongwe JB baada ya kuonekana amekopi filamu ya kihindi na kuiita mzee wa swaga wakati hicho kitendo ni cha kawaida kwenye sanaa duniani na JB sio mtu wa kwanza kukupi filamu za nje

Amesema wasanii wakubwa pia kama marehemu Kanumba na Ray nao wamewahi kukopi filamu za nje tena mpaka majina tofauti na alivyofanya JB kuchukua tu stori,na ikumbukwe ukikopi ukafanya vizuri basi hiyo ndio sanaa maana wengi wanakopi lakini hawafanyi vizuri ila JB amefanya vizuri
Hapo juu ni baadhi ya filamu za kizungu ambazo marehemu kanumba na ray walizikopi stori mpaka majina,
Picha-Rachel akiwa na Zamaradi.

No comments: