Thursday, 12 March 2015

Watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha na 23 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea katika eneo la Changarawe mafinga.

Zaidi ya abiria Arobaini wa basi la kampuni ya Majinja linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es Salaam wamefariki dunia kwenye ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Changarawe wilayani Mufindi huku abiria wengine 22 wakijeruhiwa baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na lori namba T.689 APJ mali ya kampuni ya Cipex ya Dar es Salaam lililokuwa limebeba kontena.
Mashuhuda wa jali hiyo iliyohusisha basi la majinja lenye namba za usajiri T438 CDE.lililokuwa linatokea mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa lori hilo lililokuwa katika mwendo kasi ghafla liliingia kwenye mashimo makubwa ya barabarani na kupoteza mwelekeo hivyo kulifuata basi kwenye upande wake na kusababisha ajali hiyo.
Kontena lilokuwa limepakiwa katika lori la mizigo Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja na kusababisha vifo vya watu 42 na wengine kadhaa kujeruhiwa jana katika eneo la Changarawe, nje kidogo ya mji wa Mafinga mkoani Iringa
Baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na dakika 40 wamesema awali walimuonya dereva wa basi hilo kupunguza mwendo lakini hakuwasikiliza na walipofika katika eneo la Changarawe kilometa chache kutoka mjini mafinga ndipo walipokumbana na dhahama hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Asas Abri (kulia) akiwa na viongozi wengine wakiwajulia hali manusura wa ajali hiyo.
ITV imeshuhudia miili ya watu 42 ikishushwa katika hospitali ya wilaya ya Mufundi huku majeruhi sita waliokuwa katika hali mbaya kati ya 22 wakihamishiwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza amezungumzia ajali hiyo na kusema kuwa ni moja ya tukio la ajali mbaya ya barabarani kuwahi kutokea katika mwaka huu.
Miongoni mwa manusura 22 wa ajali ya basi la Majinja lenye namba za usajili T438 CED wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa Iringa kwa matibabu. Abiria 42 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Zoezi la uokoaji katika eneo la tukio lilihusisha vyombo karibu vyote yaani jeshi la zima moto na uokoaji, jeshi la kujenga taifa JKT kutoka kikosi cha 841 kj.huku uongozi wote wa mkoa wa Iringa ukikusanyika katika eneo la tukio ambapo baadhi ya wananchi walimzonga mkuu wa mkoa wa Iringa kulalamikia mashimo hayo ambayo yanaelezwa kuwepo kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (wa pili kulia) akiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ,Mwenyekiti wakamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Iringa Salim Asas Abri (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita eneo la ajali.
 MAJINA YALIYOPATIKANA HADI SASA NI:
Baraka Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule,


Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

Basi hilo lilianza safari mjini Mbeya likiwa na abiria 37. 



No comments: