Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa
Iringa, Amina Masenza kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea
Mafinga katika mkoa wa Iringa eneo lijulikanalo kwa jina la Changarawe,
ambayo imepoteza uhai wa watu zaidi ya 40 waliokuwa wakisafiri kwa basi
hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Katika salamu zake hizo, rais Kikwete amewahakikishia wafiwa wote
kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa ndugu na jamaa zao na
kuwaombea kwa mwenyezi mungu, mwingi wa rehema watu wote waliojeruhiwa
kwenye ajali hiyo wapone haraka, ili waweze kuungana tena na ndugu na
jamaa zao.

No comments:
Post a Comment