Staa wa Muziki Fid Q, ametegua mojawapo ya fumbo kutoka katika video
yake ya Bongo Hip Hop kuhusiana na mabinti wawili ambao wamewakilisha
vizuri ndani ya kichupa hicho.
Rapa
huyo ameeleza kuwa mabinti hao wawili waliotumika katika video hiyo na
kuleta tafsiri tofauti, mmoja anawakilisha muziki wa Hip Hop na
mwingine akiwa anawakilisha Bongo Flava.
Fid Q ambaye anabeba sifa ya kusuka mistari na kuunda maana katika kila anachokifanya kupitia sanaa yake, amesema akipata nafasi atachambua maana zote zilizojificha katika video hiyo, kubwa likiwa ni kuonesha mvuto wa Bongo Flava dhidi ya ule wa Hip Hop kwa kutumia warembo.

No comments:
Post a Comment