Hali ya taharuki imewapata wakazi wa
kijiji cha Park Nyigoti kata ya ikoma wilaya ya Serengeti baada ya
mahakama kutoa ruhusa ya kufukuliwa kwa mwili wa Bi. Celina Jumapili
aliyefariki dunia na kuzikwa tarehe tatu marchi kisha kuonekana utata
katika kaburi lake ambalo leo limefukuliwa na kukuta sehemu ya viungo vya
mwili wake vimekatwa vikiwemo kiganja cha mguu vidole vya mkono wa
kushoto na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa hali iliyozua mashaka
makubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.
ITV lifika katika kijiji cha Park Nyigoti wilayani Serengeti na
kushuhudia zoezi la kufukua kaburi likiendelea ambapo inadaiwa kuwa
marehemu Celina alifariki dunia tarehe mbili ya machi na kuzikwa tarehe
tatu lakini tarehe ishirini na mbili ndugu walikuta sehemu ndogo ya
kaburi likiwa limefukuliwa ndipo wakataka kuhakiki kuwa mwili wa ndungu
yao upo au umechukuliwa. baada ya kupata kibali cha mahakama wamefukua
na kukuta viungo hivyo vikiwa vimekatwa na watu wasiyo julikana.
Akielezea namna tukio ilo lilivyo tokea mama wa marehemu Celina Bi
Nyahende Kwihamba amesema tukio hilo limewaweka katika mashaka makubwa
kutokana na kijiji hicho kushamiri kwa tabia ya ushirikina na kuiomba
serikali isaidie kumaliza tabia hiyo.
Kijiji cha Park Nyigiti mara kwa mara kimekuwa na matukio ya
kikatili kwani tarehe mbili ya mwezi marchi watu watano waliuawa na
wananchim kwa kuwatuhumu kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina na
tarehe saba ya mwezi wa pili kijiji jirani cha lubanda waliuawa watu
wawili na kuchoma moto nyuma saba kwa kama tuhuma hizo hizo.
No comments:
Post a Comment