Thursday, 2 April 2015

Mbaroni Kwa Jaribio La Kumtorosha Mch Gwajima

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu kumtorosha Mch, Josephat Mathias Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Inadaiwa kuwa Machi 29 mwaka huu majira ya tisa na nusu usiku watu hao walifika hospitalini hapo kwa madai ya kwenda kumuona Mchungaji Gwajima, jambo ambalo sio la kawaida kumuona mgonjwa kwa muda huo.
Inadaiwa kuwa kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia nguvu kuingia katika chumba alicholazwa askofu Gwajima, lakini hawakuweza kufanikiwa baada ya kukamwatwa na kikosi maalum cha polisi baada ya kuwa wakifuatilia mwenendo wa kundi hilo.
Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa walikutwa na silaha ambayo ni Bastola aina ya Berreta yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu, risasi 17 za Shortgun, vitabu viwili vya Hundi (Cheque Books), hati ya kusafiria yenye jina la Gwajima Josephat Mathias yenye namba AB 544809 na vitu vingine.

No comments: