Tuesday, 12 May 2015

Young Killer azungumzia sababu ya kutonunua gari hadi leo,


Staa wa Bongo Fleva,Young Killer amesema kuwa sababu ya kutonunua gari hadi leo ni kuwa anatumia magari ya marafiki zake kwenye shughuli zake na za kisanii na kwamba pesa yake amewekeza kwenye mjengo wake anaoujenga nyumbani kwao jijini Mwanza.
Akizungumza na Clouds Fm,alisema kuwa ana uwezo wa kupata gari muda wowote akitaka kutoka kwenda sehemu yoyote ndiyo maana hana haraka ya kununua gari.
‘’Asilimia kubwa ya washikaji zangu wana magari ndiyo maana sina haraka ya kununua gari pesa yangu nyingi nimewekeza kwenye nyumba yangu ninayoijenga nyumbani kwetu Mwanza na mama yangu ndiye anayesimamia ujenzi,’alisema Young Killer. Alipoulizwa ni gharama kiasi gani ametumia kwenye ujenzi alisema kuwa bado hajajua kwani anajenga kwa mafungu atajua gharama hadi atakapomaliza ujenzi.

No comments: