Sunday, 28 June 2015

Brand New Song By TOP 20 KINONDONI TALENT SEARCH - KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO

Leo ninaomba nikushirikishe wimbo huu mpya ambao umefanywa na vijana 20 ambao wameingia katika hatua nyingine ya juu zaidi baada ya kuchujwa kutika kundi la vijana zaidi ya 17510 waliojitokeza katika usahili wa KINONDONI TALENT SEARCH 2015 pale coco beach.. hawa vijana 20 hawa ndio pekee waliopita viwango vyote na kuonekana ni waimbaji bora ambao wako tayari kwa ajili ya kuchujwa na hatimaye kumpata mshindi hapo baadae mwezi ujao..wimbo unaitwa KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO ambayo kauli mbiu hii inabeba maana nzima ya dhima na kusudi la kuanzishwa kwa mashindano haya ikiwa ni  kuhakikisha kila mkazi wa kinondoni ananufaika na kipaji chake alichopewa na Mungu.nafurahi kwani nina matumaini kwa nafasi yako uliyonayo utaifanikisha nyimbo hii kuwafikia wasikilizaji wote Tanzania kwani hata hivyo ujumbe ulioko katika wimbo huu unawahusu vijana wote Tanzania walioo na ndoto zao mtaani kupitia vipaji vyao.. ila wamekata tama hawajui wapi waanzie.. vijana wenzao wameona wawape moyo kwa wimbo huu maalumu..
NAKUOMBA KWA NAFASI YAKO NISAIDIE KUUFIKISHA WIMBO HUU KATIKA MASIKIO YA WASIKILIZAJI WAKO WALIO WENGI.
Jina la wimbo – KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO
Mtunzi/composer – PETER MSECHU
Mpangilio wa mziki/music director – PETER MSECHU
Studio live recording – REAL STUDIO
Producer – MASANJA

No comments: