June 07 2015 mmoja kati ya Viongozi
ambao wameingia kwenye headlines za kutajwa kwamba na yeye anahitaji
kusogelea njia ya kuingia Ikulu ya TZ kwenye Uchaguzi wa mwaka huu 2015
ni Naibu Waziri, January Makamba.
Tayari kathibitisha kwamba ana lengo hilo, kutoka Mlimani City Dar hapa nina nukuu ya baadhi ya sentensi zake wakati akitangaza nia hiyo.
“Nimeona
nitumie siku ya leo kuwajulisha kwamba nimeamua kuomba nafasi ya Rais wa
Tanzania… keshokutwa nitakwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuomba ridhaa
ya CCM ili niteuliwe kugombea mwaka huu.. Naelewa kiu ya Watanzania
kupata aina mpya ya uongozi utakaotoa matumaini mapya yatakayozaa
Tanzania mpya“>>>
“Siko
mbele yenu leo kuwasimulia matatizo ya Watanzania.. niko mbele yenu
kueleza tutakavyotatua matatizo ya nchi yetu. Nitaunda Serikali ya
Mawaziri wasiozidi 18, haitakuwa na mtu hata mmoja anaetiliwa shaka
kuhusu uadilifu wake wala uwezo wake“>>>
“Kwenye
Serikali yetu tutataka kila mtu afuate Sheria za nchi hata ziwe ndogo
kiasi gani.. Tutakabiliana na tatizo la ubadhilifu wa mali za umma kwa
nguvu zetu zote“>>>
“Viongozi
wengi wa siasa wameliita tatizo la ajira kuwa ni bomu lakini kulielezea
tatizo la ajira sio kulitatua.. tukiwezesha 80% ya biashara ndogondogo
hapa nchini zitakuwa zimepunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la
ajira”>>>
“Tutaongozwa na dira ya elimu inayochochea vijana kujiajiri“>>>
“Ualimu ni wito, hatutaki ualimu uwe adhabu.. Tutazitatua changamoto za Walimu, hatutaingiza Siasa kwenye elimu“>>>– January Makamba.
Isikilize Hotuba ya January Makamba iko hapa ,











No comments:
Post a Comment