Friday, 31 July 2015

BASATA WAMFUNGIA SHILOLE KWA PICHA ZA AIBU.


Serikali kupitia baraza la sanaa (BASATA), limemfungia msanii wa muziki na mmiliki wa hits kadhaa ikiwemo ‘Nakomaa na jiji’ kutojishughulisha na kazi za sanaa kwa mwaka mmoja kwa kile walichokiita ukosefu wa maadili.
Barua kutoka BASATA ilianza kusambaa toka jana saa 4 za usiku, ikiainisha chanzo kikuu ni sehemu ya picha katika ‘show’ aliyoifanya Shilole May 9 mwaka huu nchini Uholanzi.

Yapitie hapo chini maneno yaliyoandikwa na basata kwenye barua hiyo, ‘then’ tuachie maoni yako.kwenye Acc zetu za Tweeter>>>https://twitter.com/KaysonNgessa NA Facebook>>>>https://www.facebook.com/Ngessakinollo

 “Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili.
 BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani,
BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako,
Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi.
Umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae”.

No comments: