Saturday, 11 July 2015

MUNGU MKUBWA, BANZA ATOKA HOSPITALI

Mwanamuziki wa Dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone.
Banza aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo, Jumatano iliyopita ambapo kwa mujibu wa kaka yake ana nafuu japokuwa bado hali si shwari kwani daktari aliyekuwa anamtibu aliwaeleza kwamba ndugu yao huyo ana tatizo la upungufu wa damu.
“Tunamshukuru Mungu mgonjwa wetu ameruhusiwa japo bado hali yake haijatengamaa kwani tofauti na matatizo ya awali ya fangasi za kichwani, anakabiliwa na upungufu wa damu hivyo tumeshauriwa tumpe vyakula vya kuongeza damu,” alisema Hamis.

No comments: