Zimebaki kama wiki mbili hivi ugeni wa
White House utue pale Jomo Kenyatta International Airport, Nairobi Kenya
kama ambavyo iliahidiwa.
Safari ya kihistoria ya Rais Obama
ndani ya Kenya inakaribia, huu ni uthibitisho mwingine kwamba mambo
yameiva… Gari za watu wa Usalama tayari zimeshushwa Nairobi na pia kuna
Helicopter zaidi ya nane za Kijeshi tayari zimetua.
Mbali na gari hizo pamoja na helicopter zilizotua, wako Maofisa Usalama
zaidi ya 200 ambao tayari wako Kenya kwa ajili ya kuhakikisha mpaka siku
Rais Obama anatua kunakuwa na usalama wa kutosha.
Stori nyingine kutoka Nairobi inaonesha timu ya watu wa Usalama watakuwa
kama 800 hivi kutoka Marekani na Polisi zaidi ya 2,000 wa Kenya
watahusika na Ulinzi wa msafara wa Obama akiwa Kenya.
![]() |
| The Beast’ ya Rais Obama na Helicopter juu vitakuwa Nairobi time yoyote kuanzia sasa hivi. |





No comments:
Post a Comment