![]() |
| Bw Martine Shigela |
Ikumbukwe kuwa Shigela aliwahi kuwa katibu mkuu wa UVCCM. Anachukua nafasi ya ya Rajab Luhwavi ambaye ameteuliwa majuzi kuwa Naibu katibu mkuu CCM Bara, kuchukua nafasi ya Mwigulu Nchemba aliyejiuzulu.
Aidha, rais Kikwete pia amemteua Bw. Jumaa George Bwando kuwa MNIKULU mpya, akichukua nafasi ya Shaban Gurumo aliyeondolewa majuzi pia.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wasaidizi wake wawili. Uteuzi huo unaanza mara moja.
Katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Bwana Jumaa George Bwando kuwa Mnikulu. Bwana Bwando ni mtumishi wa miaka mingi wa Serikali.
Rais pia amemteua Bwana Martine Shigela kuwa Msaidizi wa Rais (siasa). Bwana Shigela anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajab Luhwavi ambaye karibuni aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
9 Julai, 2015

No comments:
Post a Comment