Jeshi la polisi kupitia oparesheni kali ya kupambana na makosa mbalimbali ya kihalifu kwa kutumia silaha za moto limefanikiwa kukamata silaha zilizokua zimeporwa katika kituo cha polisi cha Stakishari jijini Dar es salaam. Katika matukio mawili tofauti ambapo mnamo tarehe 17 mwezi wa 7 jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna kikundi cha uhaalifu kimejipanga kufanya uhalifu huko Temeke eneo la Tuangoma .
Ndipo kikosi maalum cha jeshi hilo kiliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watu watano baada ya majibizano ya risasi na watu hao, huku watu watatu wakijeruhiwa kwa risasa na kufariki njiani walipokuwa wakiwaishwa hospitali.
Katika mwendelezo wa oparesheni hiyo kulipatikana taarifa za kuaminika kwamba silaha zilizoporwa katika kituo cha polsi cha Stakishari zimefichwa mkoa wa Pwani katika kijiji cha mandimkongo kata ya bupu wilaya ya Mkuranga ndipo jeshi hilo likafanya msako mkali na kufanikiwa kupata silaha 15 ambazo ni mali ya kituo cha Polisi Stakishari na kukuta kiasi cha fedha cha shillingi millioni 170 zilizofungwa kwenye sanduku maalum.
Aidha naibu kamishina wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ametoa wito kwa wananchi na wanahabari kuendela kusaidia jeshi hilo katika utoaji wa taarifa zonazohusu matukio ya uhalifu ili kukomesha vitendo hivyo.



No comments:
Post a Comment