![]() |
| Mjukuu wa Nelson Mandela, Mbuso Mandela{25YRS} |
Historia ya Nelson Mandela ni historia ya kishupavu iliyosimamia ukweli, usawa na haki na pale mtu anapojaribu kuweka doa kwenye jina la familia ya Nelson Mandela watu hawatakuelewa kabisa. Mjukuu wa Nelson Mandela, Mbuso Mandela mwenye miaka 25 anaziandika headlines South Africa baada ya kesi ya ubakaji wa msichana wa miaka 15 dhidi yake kufikishwa Mahakamani.
Kwa taarifa zilizotolewa na ripoti iliyofikishwa polisi zinasema kuwa Mbuso Mandela alimshambulia binti huyo wakati wakiwa kwenye restaurant moja maarufu jijini Johannesburg… na wakati akiwa anapata chakula cha jioni na marafiki zake msichana huyo aliinuka kwenda msalani ambako Mbuso alimfuata nyuma kumshambulia na kumbaka.
Mbuso alifikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu jijini Johannesburg kusikiliza mashitaka hayo lakini polisi wamesema mjukuu huyo ya kiongozi mkubwa wa Africa ataendelea kushikiliwa na polisi mpaka tarehe yake ya kutolewa dhamana itakapotajwa.
![]() |
| Mke wa kwanza wa Mwanaharakati Nelson Mandela,Bi,Winnie Mandela. |
![]() |
| Hayati Nelson Mandela"Madiba" |





No comments:
Post a Comment