Staa wa Bongo movie Batuli, siku ya jana alipatwa na ajali ya kuunguliwa nyumba yake kwa moto wakati akiwa kwenye miangaiko yake ya kila siku katika uzinduzi wa kampeni za CCM uliyofanyika jana Jangwani Dar es salaam.
Batuli amefunguka kwa njia ya simu kuwa....
"Watu wengine wamehusisha swala hili na mambo ya chuki za kisiasa lakini mie namshukuru Mungu hakuna aliyepoteza maisha ama kujeruhiwa katika ajali hii, ndani kulikuwa na mtoto wa ndugu yangu lakini jirani walivunja vioo na kumnusuru lakini mali hakuna nilichookoa zaidi ya magari yangu tu"
Alisisitiza Batuli.


No comments:
Post a Comment