Watu
tisa waliokuwa wakisafiri na gari dogo aina ya Noah yenye usajili namba
T812 BJU, wamefariki dunia papo hapo baada ya gari hilo kuacha njia na
kupinduka.
Ajali hiyo imetokea saa 11 jioni katika kijiji cha Mwamanga wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza kwenye barabara kuu ya kutoka shinyanga kuelekea mwanza, wakati gari hilo kumshinda dereva wake ambaye ni Koplo Mstaafu wa Jeshi, Moris Lukenza, mkazi wa Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo , Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Charles Mkumbo, amesema gari hiyo imepata ajali jana jioni kufuatia mwendokasi wa dereva uliomsababishia kushindwa kulimudu gari na kisha kupinduka.
Aidha, Kamanda Mkumbo amesema katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi sita ambao hali zao zimeelezwa ni mbaya na wamehamishwa hospitali ya rufaa Bugando Jijini Mwanza

No comments:
Post a Comment