Sunday, 6 September 2015

ATIMAYE JACKLINE WOLPER AVISHWA TENA PETE FEKI NA KIDUME.

Utata waibuka Baada ya Wolper Kuvishwa Pete

 

Baada ya hivi majuzi staa wa Bongo Movies,  Jacqueline Wolper  ‘Jacqueline Lowassa’ kuweka picha mtandaoni akivishwa pete na mchumba wake,siku  ya jana kumeibuka  habari za udaku sambamba na picha zikimuonyesha jamaa huyo aliyemchumbia Wolper akiwa kwenye kwenye vazi la harusi na mwanamke ambaye inasemekana ni mkewe.

Habari hizo ambazo hazijathibitishwa na jamaa huyo wala Wolper zinadai kuwa jamaa ni mume wa mtu wa  ndoa  ya mwaka 2014 nchini Congo na kwa sasa mkewe yupo nchini humo akiwa hana taarifa yoyote juu ya uchumba huu wa mmewe.

No comments: