Mgombea urais wa UKAWA Mh.Edward Lowasa amefanya mikutano ya kampeni
katika majimbo matano ya mikoa ya Kigoma na Tabora na kuwawaomba
wananchiwa maeneo hayo kuungana na watanzania wengine wanaopenda
mabadiliko kumchagua rais,wabunge na madiwani wa vyama vya UKAWA ili
kurahisisha kazi ya kuondoa kero zinazowakabili.
Akizungumza katika mikutano hiyo Mh.Lowasa amesema kazi ya
kukabiliana na changamoto zinazoandamana wananchi kwa muda mrefu iko
ndani ya uwezo wake na viongozi wenzake wa ukawa na itakuwa nyepesi
zaidi kama wananchi watatoa ushirikiano.
Mh.Lowassa ambaye ameweza kuwafikia wananchi wengi wa vijijini
baada ya kuanza kutumia HELCOPTER amesema UKAWA imejipanga kikamilifu na
kutumia sera zilizoko kwenye ilani ya kutatua kero nyingi
zinazowakabili wananchi kinaachotakiwa sasa ni ushirikiano wa wananchi.
Viongozi na makada wengine wa UKAWA walioambatana na mgombea
wamewaomba wananchi kuwachagua viongozi wa UKAWA wakiwemo madiwani na
waabunge ili kutimiza lengo la mabadiliko.
Mh.Lowassa anaendelea na kampeni katika majimbo ya mkoa wa Tabora na baadaye Shinyanga.
|
No comments:
Post a Comment