![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba |
Katika
taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari imemtaka mgombea urais
kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mh. John Magufuli kufuta kauli zake
ikiwemo ya kufanisha mchakato wa uchaguzi na vuguvugu la mabadiliko ya
Libya pamoja na serikali yake kuwapiga risasi wahalifu wa kutumia
silaha.
Mh. Magufuli mnamo tar 28 Agosti akiwahutubia wakazi wa Mbalizi Mbeya vijijini alisema “Msitoe hukumu ya jumla zipo nchi zilifanya hivyo zilijuta,Libya ya Gadafi ilikuwa ukioa unapewa nyumba, unatafutiwa mtaji ,elimu na umeme bure lakini wananchi walichoka raha.....wakasema wanaondoka lakini wale vijana waliosema wanataka raha na wale vijana waliosema wanataka ukombozi wa haraka ndio wa kwanza kuvuka bahari ya Mediteranian kwenda Ulaya."
Kituo hicho kimesema kauli hizo zinatoa vitisho kwa wapiga kura kinyume na demokrasia kwa kuwa huwezi kufananisha mabadiliko ya kimapinduzi ya Libya na umwagaji damu uliotokea huko na mabadiliko ya amani kwa kupitia mchakato wa uchaguzi za kidemokrasia.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa kauli hizo za mgombea huyo ni za kukemewa kwa kuzingatia nchi na chaguzi zinaongozwa kikatiba na Katiba inakinzana kabisa na kauli zilizotolewa na kiongozi huyo.

No comments:
Post a Comment