Monday, 28 September 2015

LOWASSA:-SERIKALI ISIJARIBU KUVURUGA UCHAGUZI.

Serikali imetakiwa kutokujihusisha na mpango wowote wa kutaka kuvuruga zoezi la uchaguzi mkuu kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kwani kufanya hivyo ni hatari na kunaweza kuvuruga amani ya nchi.
Akihutubia maelfu ya wakazi wa jimbo la Vunjo mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe ameonyesha kusikitishwa kwake na kile kinachodaiwa ni mbinu chafu zinazofanywa na CCM za kutaka kuvuruga uchaguzi mkuu kwa kujaribu kuvuruga utendaji wa tume ya taifa ya uchaguzi.
Akiwa mjini vunjo Edward Lowassa amehutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Kahe, Kirua na Himo ambapo amewataka watanzania kuhakikisha wanampigia kura nyingi tena za kishindo na kwamba serikali atakayoiinda itajikita katika kusimamia rasilimali za nchi.

No comments: