Monday, 28 September 2015

MAHUJAJI WALIOFARIKI KWENYE AJALI MECCA KUZIKWA HUKO HUKO.


Zaidi ya Mahujaji 700 walioripotiwa kufarika baada ya maafa yaliyotokea katika mji wa Mina – Makka wakati wa kufanya ibada ya hija, siku ya alhamis wiki iliyopita.
Hali ya wasiwasi ilitanda kwa Ndugu, Jamaa wa taifa la Tanzania kwa ujumla kutaka kujua je ni watanzania wangapi waliohusika kwenye tukio hilo ?
 Mapema leo asubuhi akizungumza na kituo cha runinga cha Azam tv Afisa Habari wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE ), Khamis Tembo amesema Mahujaji Wanne wanaotoka Tanzania wamedhibitishwa kufariki katika tukio hilo.
Hamis Tembo ameeleza kuwa Mahujaji hao watazikwa huko ikiwa ni kama utaratibu na imani ya kufuata matendo ya Mtume MUHAMMAD (S.A.W) .
Kwa mujibu wa afisa habari huyo amesema Mahujaji wameshaanza kurudi katika nchi zao na kundi la kwanza la Mahujaji 40 wanatarajiwa kutua Tanzania leo saa tano asuhuhi na watashuka kwenye kiwanja cha Karume huko Zanzibar, huku kundi la pili likitarajiwa kufika tarehe 4 mwezi wa 10. Tembo amesema mwaka huu taasisi 22 zimesafirisha zaidi ya watanzania 2100 kwenda kufanya ibada ya Hijja huko Makka nchini Saudi Arabia.

Yaaa ALLAH please forgive them....

"Allahumma ghfirlaha wa rhamha,wamaskanah filjanna,....
AMIIN THUMMA AMIIN.."
 
Yaaa ALLAH please forgive them....

"Allahumma ghfirlaha wa rhamha, Wamaskanah Filjanna,....
Thumma amiin amiin.."

No comments: