![]() |
| Emmanuel Mbasha na Masanja Mkandamizaji. |
Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa wiki iliyokwisha ambapo Mahakama hiyo ilimwachia huru Emmanuel Mbasha baada ya kumuona kuwa hana hatia juu ya Shitaka hilo.
Kupitia Acc yake ya Facebook Mbasha aliandika maneno yaliyohusiana tukio hilo muhimu maishani mwake......
Waweza kuyasoma maneno hayo hapo chini......
Jumapili ya Jana 27,katika kanisa la mito ya baraka chini ya mchungaji wangu Askofu Mwakibolwa ilikua ni Siku yangu ya kipee kutoa sadaka ya shukrani mbele za Mungu kwa matendo makuu aliyonifanyia ninakila sababu ya kusema asante Mungu mana umenivusha ktk mapito magumu niliyokuwayo na hila za adui na kuniepusha na kifungo cha maisha segelea,nasema asante sana Mungu wangu kweli mipango ya shetani imeharibika kwa jina la Yesu kristo.na nimekutumaini Mungu sikukuacha kipindi chote cha mapito Yangu nimekua nikifunga na kuomba na kulia mbele zako Mungu kweli nimeamini Mungu unajibu maombi tena kwa wakati,napenda niwashukuru wadogo zangu ambao wamekua bega kwa bega na mie pia jana nilikua nao kanisan,pia baba Yangu Mzazi pamoja na mama.nawashukuru sana mawakili wangu.ninapenda niwashkuru rafiki zangu wote yani wote yani wooooteeee ambao mmelia pamoja nami mmekua mkinitia moyo nk nasema asanteni sanaa.zaidi tuendelee kuombeana hata wewe unayepita kwenye majaribu sasa usimwache Yesu endelea kumwamini na kuomba kwa bidii atakuvusha tu amini hivyo daima.huu wimbo nilisimama nao ktk kuharibu mipango ya shetani korasi haribu mipango ya shetani haribu, vunja vunjaaa haribu haribu haribu hamipango ya shetani weeeeeeeee.imeharibika yoteeeeeeee.....maisha yanaendelaaa
NB:-PICHA zaidi kwenye tukio hilo,
![]() |
| Mtumishi wa MUNGU Emmanuel Mbasha akiwa na Mtumishi wa MUNGU Emmanuel Mgaya Maarufu kama "Masanja Mkandamizaji." |
![]() |
| Askofu Mwakibolwa wa Kanisa la Mito ya Baraka akimuwekea mikono ya Baraka Mtumishi wa MUNGU Emmanuel Mbasha. |











No comments:
Post a Comment