Wednesday, 23 September 2015

NAY WAMITEGO AWASHUKIA WASANII WANAOKASHIFU WAGOMBEA WAKATI WA KAMPENI.

Zikiwa zimebakia siku 31 kuelekea uchaguzi mkuu, msanii Nay wa Mitego amendika Mtandaoni maneno ya kuwahasa Wasanii wenzake wanaopiga Kampeni za Kukashifu Wagombea kuwa wasisahau kuwa kuna Maisha baada ya October 25,jambo lililowahi kuongelewa pia na Msanii wa Maigizo Haji Adam "Baba Haji" wiki iliyokwisha.
Nay Wamitego na Baba Haji wote wameungana pamoja wakimsapoti mgombea kupitia UKAWA Mh,Edward Ngoyai Lowassa anayegombea Urais{UCHAGUZI MKUU 2015}kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo{CHADEMA}

"Wasanii tubaki kua wahamasishaji tu!Kuanza kukashfu Viongozi utadhani labda nawewe umekua mwana Siasa au Mgombea itakuja kutu Cost baadae. Hua najiuliza cjui wanalipwa shiling ngapi maana wanasahau wao ni wasanii na wana Mashabiki wenye Imani tofauti, pia kuna Maisha baada ya uchaguzi. Endeleeni kutumika vibaya kwa Njaa ya leo na kwa maslahi ya wachache na kusahau kuna kesho. Pigania unacho amini but si kwa kashfa wala Matusi. Mimi naamini #Mabadiliko2015 .Tukutane #October25" ...
Ameandika hivyo Nay wa Mitego
Chanzo-EATV

No comments: