Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephath Gwajima (katikati) akizungumza kwenye mkutano na Wanahabari katika Hoteli ya Land Mark.
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo amefunguka kuhusu tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema) Dkt. Willbrod Slaa na kusema kiongozi huyo ni muongo, akidai madai yote dhidi yake hayana ukweli wowote.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari na baadhi ya waumini na wachungaji wake kwenye Hoteli ya LandMark jijini Dar es Salaam, alisema amelazimika kuweka mambo wazi kwa kuwa kiongozi huyo kushindwa kuwa mkweli.
Alisema chanzo cha Dkt. Slaa kuondoka Chadema si ujio wa Edward Lowassa kujiunga na chama hicho, bali aliyesababisha ni mkewe aliyemtaja kwa jina la Josephine. | |
No comments:
Post a Comment