![]() |
mkuu wa idara ya habari wa shirikisho TFF Baraka Kizuguto |
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kupitia kwa mkuu wa idara ya habari wa shirikisho hilo, Baraka Kizuguto ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuelekea mchezo wa Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles mechi itakayopigwa jumamosi ya Seotemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
“Kocha
amefurahi kuwapokea wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta, Thomas
Ulimwengu na Mrisho Ngassa na kwa hizi siku zilizo bakia, ana imani
kabisa atafanya maelekezo ya mwisho na wachezaji wengine kuelekea mchezo
huo, ana imani timu itafanya vizuri”>>> Kizuguto
Hata hivyo kwa upande wa timu ya taifa ya Nigeria bado haijatoa taarifa rasmi inakuja na msafara wa watu wangapi na muda itakao wasili Dar Es Salaam, ila kupitia kwa afisa habari wao ni kuwa timu itawasili Dar Es Salaam kwa ndege ya kukodi na kuna uwezekano wa kufika Dar Es Salaam saa 4 usiku Septemba 3. Waamuzi wa mchezo huo ni kutokea Rwanda watawasili Septemba 3. Muamuzi wa kati ni Luis Hakizimana wasaidizi ni Onole Simba, Jean Bosco Tegeka na muamuzi wa akiba ni Abdul Karim Twagilamuzika na Charles Kasembe kutokea Uganda.
Zaidi msikilize Kizuguto
No comments:
Post a Comment