![]() |
Moto unaoendelea kuwaka Mlima Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha. |
![]() |
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Martin Loibooki akiongea na wanakijiji wa
Olosinoni wanaoshiriki zoezi la kuzima moto unaonendelea kuwaka Mlima
Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana.
|
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

Moto
mkubwa umezuka mwishoni mwa wiki hii na kuunguza sehemu ya Mlima Meru
katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa
chanzo cha moto huo ni vitendo haramu vya urinaji wa asali ndani ya
msitu wa hifadhi hiyo.Wananchi wapatao 200 kutoka vijiji jirani vya Olosinoni na Kisimiri
Juu wakishirikiana na TANAPA wamefanikiwa kuudhibiti moto huo ili
usiweze kuleta madhara makubwa kwa binadamu hususan wageni wanaotembelea
hifadhi kwa lengo la kupanda Mlima Meru.
Hadi
sasa hakuna wageni waliodhurika na moto huo na tahadhari zote
zimechukuliwa ili kudhibiti madhara zaidi kwa binadamu na shughuli za
utalii ndani ya hifadhi.
Shirika
la Hifadhi za Taifa linaendelea kuwatahadharisha wananchi juu ya
vitendo vya kuingia ndani ya hifadhi bila kibali kwa shughuli ambazo
zinaweza kuwa chanzo cha kuzuka kwa mioto hii ambayo husababisha
uharibifu wa mazingira pamoja na kuharibu vyanzo vya maji.
Aidha,
katika kuhakikisha kuwa moto huo unadhibitiwa kwa haraka, TANAPA
imeongeza nguvu kazi ya wananchi wakishirikiana na vyombo vingine vya
dola ili kuweza kuudhibiti moto huo.
Mwisho,
taarifa kamili juu madhara yaliyosababishwa na moto huo itatolewa mara
baada ya kukamilika kwa zoezi la kuzima moto na umma utaendelea kupewa
taarifa ya maendeleo ya zoezi la uzimaji wa moto kila wakati.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
21.09.2015
dg@tanzaniaparks.com
www.tanzaniaparks.com
No comments:
Post a Comment