![]() |
| Msanii aliyewahi kubamba kwa staili ya Tanzania, Kenya na Uganda (Takeu), Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ akiugulia kitandani baada ya kulishwa inachodaiwa kuwa ni Sumu. |
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na staa
huyo aliyewahi kubamba na nyimbo nyingi zikiwemo Kikulacho na Fagilia,
Mr. Nice alikuwa Kahama, Shinyanga katika kampeni za mgombea ubunge wa
Jimbo la Kahama, James Lembeli.
![]() |
| Mr. Nice |
“Ujue tangu Lembeli (James) yupo Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Mr. Nice alikuwa mmoja wa watu wake wa karibu katika
kumfanyia kampeni na kwa kipindi hiki ambacho Lembeli yupo Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amekuwa akiambatana naye kwenye
kampeni. Kwa hiyo kulishwa kwake chakula chenye sumu huenda ni bahati
mbaya,” kilisema chanzo.
Amani lilimvutia waya Mr. Nice, kujua
zaidi hali yake ambapo alikataa kuweka wazi suala hilo kwa sasa kutokana
na washauri wake kumsihi hivyo kwa kipindi hiki alichokuwa nacho.
Naye rafiki yake wa karibu aliyewahi
kuingia naye katika malumbano, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ aliweka wazi
kwa sasa hana mawasiliano na Mr. Nice lakini mwaka 2010 alifanya naye
kampeni hukohuko Kahama za Lembeli.
Alipotafutwa Lembeli kuongea juu ya hili tukio, simu yake iliita bila kupokelewa.
Hivi karibuni, Mr. Nice kupitia mtandao
wake wa Facebook, aliwashukuru mashabiki, familia na madaktari wake
pamoja na Lembeli waliopigania kuokoa maisha yake.


No comments:
Post a Comment