Sunday, 11 October 2015

Aika na Nahreel{Navy Kenzo}na mpango wa kuwa Mume na Mke.

Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo ‘Nahreel na Aika’ ambao pia ni mtu na mpenzi wake wamezungumzia mpango wao wa kufunga ndoa.
Nahreel na Aika wamesema mpango upo ila hawajapanga ni lini haswa utakamilika, ” Yeah ndoa ipo,ipo kabisa, hatuwezi kusema sasa hivi lakini itafika tu muda mzuri wa kufunga ndoa
Navy Kenzo walikuwa miongoni mwa wasanii waliofanya show kali kwenye fainali za shindano la kutafuta vipaji la Bongo Star Search juzi ambapo mshindi wa Shindano hilo alikuwa ni kijana Kayumba Juma.

No comments: