Saturday, 10 October 2015

Anayetuhumiwa kusambaza uzushi kumhusu Gen. Davis Mwamunyange apandishwa kizimbani.

-Anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Davis Mwamunyange, Benedic Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza Kulia) apandishwa kizimbani

-Anatuhumiwa kwa makosa ya mtandao.


Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao anayetuhumiwa kusambaza katika mitandao taarifa za uongo zinazomhusu mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Benedic Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza Kulia) akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka.

Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini(wa Pili kulia), Huang Kun Bing (26)Raia wa China (wa Tatu Kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza Kushoto) Hefeez Irfan (32)(wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig(41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakam ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka ya Uwizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network).

Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23. watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.

No comments: